Duration 2:56:49

Mahojiano ya Rais Magufuli na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu

34 139 watched
0
122
Published 4 Nov 2016

Rais Magufuli: Niwashukuru sana kwa michango yenu mikubwa katika maeneo yenu ya kazi. Amesema anahisi ametimiza malengo kwani makusanyo yameongeza kutoka bilioni 800 mpaka 1.2. Anagusia suala la ndege, anasema haiwezekani kujenga utalii bila ndege za uhakika. Kasema sasa ziko tatu na nyingine itakuja mwezi wa sita, mwisho jumla zitakua saba. Anagusia flyover ya Tazara. Kuhusu kilimo, anasema wawekezaji wameshaanza kuja na wakulima wameshaanza kuona matunda ya kuweka maelekezo mazuri katika kilimo. Anatolea mfano kilimo cha korosho kuwa bai ya korosho imetoka Tshs 1000 mpaka 4000 kwa kilo. Pia Pamba bei imeongezeka. Kuhusu nishati bajeti ya mwaka huu ni trilioni 1.3 na anaongelea mradi wa nishati wa Kinyerezi. Elimu, bajeti ya elimu mwaka huu 4.47, wakati anaingia bajeti ya elimu bure haikuwepo lakini walitoa extra ya makusanyo kugharamia elimu bure japo ina changamoto zake ikiwemo kuongezeka kwa en 84 26 Bajeti kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi imeongezeka kutoka bilioni 340 mpaka 473 na wanafunzi wameongezeka kutoka 98,000 mpaka 124,320. Tulipochukua hatua za kuwakopesha wanafunzi wengi zimejitokeza changamoto ikiwemo wanafunzi hewa, katika maendeleo yoyote changamoto huwa zipo. Mfumuko wa bei umeshuka kutokea asilimia 7 hadi 4.5, watu watauliza hela mbona hazipo na zitaendelea kutokuwepo kwa watu ambao ni wapiga dili. Tuna helium na nchi zenye madini hayo ni tatu tu duniani, pia graphite hivyo nchi hii ni tajiri sana. Kulikuwa na safari za hovyo hovyo za watu kupishana angani na nimeanza mimi, nilialikwa mikutano 47 ila nimeenda 3. Pamoja na kufanya hivyo bado marafiki zetu wametuheshimu na kuja kututembelea. Tumepanga Tanzania kuwa ya viwanda, wawekezaji wapo, kwa maoni yangu ninaona tunaenda vizuri katika kuwatumikia watanzania. Nisije kumaliza maswali, asante sana. Swali-Tido Mhando: Ulichukua muda kuunda baraza la mawaziri, Je Katika tathmini hiyo wanafanya kazi kulingana na ulichotegemea wakifanye Jibu-Magufuli: Serikali niliyonda imenisaidia sana na wanafanya kazi zao vizuri, niliona niwe na baraza la watu wachache katika kuwatumikia wananchi, changamoto zipo lakini nina imani kubwa. Swali-Lulu Sanga TV 1: Kuna changamoto kubwa sana ya dawa, watoto wengi wanakufa kutokana na kukosa dawa, unaoneje ukibana matumizi kupata dawa ukazigawa hospitali kubwa au kampeni kama ile ya madawati. Jibu-Rais Magufuli: Katika bajeti yetu tumetenga bilioni 1.99 na tumeongeza bajeti ya kununulia madawa karibu mara kumi. Tumebadilisha utaratibu badala ya kununua kutoka kwa suppliers sasa tunanunua moja kwa moja kutoka viwandani pia kuna nchi zinataka kuwekeza kujenga viwanda vya kutengeneza madawa hapahapa. Swali-Edoni Mwanika: Kwa nini miswada ya habari inakuwa haipewi muda wa kutosha kujadiliwa na huletwa kidharura tu? Jibu-Rais Magufuli: Sheria yeyote ina misingi yake, mchakato wa sheria hizi umeanza mwaka 2010 hadi mwaka huu, hakuna muda sahihi ungetosha kujiandaa. Hata hivyo hili ni suala ambalo lipo ndani ya maamuzi ya bunge hivyo siwezi kuingilia, Punde musuada huu utakaponifikia nitaisaini na kama ni marekebisho yatafuta. Swali-Frank: Umeokoa kiasi gani kwa kutosafiri nje? umechukua hatua gani kuhakikisha ukandaa wa Afrika mashariki unakuwa salama? Suala la diaspora wana Jibu:Fedha tulizookoa ni mabilioni, hata hivyo siyo kwamba hatusafiri kabisa ili tunahakikisha kunakuwa na uwakilishi ambao unapunguza gahrama. Tumekuwa tunashughulikia migogoro inayoendelea, DRC nimemtuma mwenyekiti wa mawaziri kwenda ili kutafuta suluhu. Suala la migogoro linadiliwa mezani, Burundi tumemteua Mh Mkapa na anasuluhisha na mambo yanaenda vizuri. Swali-Sanga: Una maoni gani katika ishu ya Zanzibar na Utawala bora? Jibu-Rais Magufuli: Hali ya Zanzibar wamefanya uchaguzi wao vizuri na Dr shein anafanya vizuri na mambo yanaenda vizuri Swali-Manyere: Msimamo wetu kuhusu Morocco; Je Ikulu haiwezi kuandaa tuzo kwa waandishi wanaondika mambo mazuri kuhusu nchi? Jibu-Magufuli: Tanzania ni nchi isiyofungamana na upande wowote na hivyo tuna uhuru wa kushirikiana na nchi yeyote. Hata hivyo Moroco tunashirikiana na nao katika kukuza biashara Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri kwelikweli, Nashirikiana na kila mtu hata Masoud anavyonichora kichwa kimevimba hapa, nashirikiana naye. Swali:Pasco Mayala: Ulitumia mamlaka gani kuamuru bunge na mahakama kufanya unayoyataka? ulitumia mamlaka gani kuzuia mikuatana ya kisiasa? Jibu: Serikali ndiyo inahusika na kugawa fedha zote kupitia bajeti, fedha zikitumika vibaya anayehusika ni serikali. Mungu awabariki sana

Category

Show more

Comments - 21