Duration 12:48

EXLUSIVE: Utata Mapipa 4,280, KINGO ZA ZEGE 474 barabara ya Morogoro, watumiaji waomba yaondolewe

2 429 watched
0
5
Published 28 Jun 2021

Kwa mtumiaji wa Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kibaha, bila shaka umewahi kusikia malalamiko juu ya mapipa na kingo za zege zilizowekwa pembeni na hata katikati ya barabara kama vizuizi wakati ujenzi ukiendelea. Mapipa hayo takribani 4,280 na kingo za zege 474 yamekuwa yakisababisha adha mbalimbali kwa watumiaji wa barabara hiyo, ikiwemo kubadili uelekeo wa barabara kila baada ya muda na kusababisha usumbufu wa mara kwa mara. Hata hivyo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Dar es Salaam (Tanroads), Eliamin Tenga anasema mapipa hayo yapo kwa sababu kuna baadhi ya vitu havijakamilika na ni suala la muda tu.

Category

Show more

Comments - 3