Duration 32:3

Salama Na Nizar Ep 23 | RAHA LEO KUCHELE Part 1

22 299 watched
0
199
Published 5 Jul 2020

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru� �� GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Wakati Vancouver White Caps wanamtaka Nizar Khalfan baada ya kumuona akiwa anakipiga hapa nyumbani wakati yuko na timu ya Taifa ya Tanzania haikua habari au jambo la kushangaza miungoni mwa wachezaji na walokua wakimuona na kumfahamu mchezaji huyo vizuri. Kila mtu kati ya hao alikua akiomba ki vyake kijana huyu kutoka Kusini mwa Tanzania apate nafasi ya kwenda kuwakilisha Taifa na kuendeleza kipaji chake maridhawa kabisa. Nizar ametokea Mtwara na kwenye familia yake kwa mujibu wa maongezi yetu Mzee wake alikua akiupiga ingawa si mwingi kama wa Master Chef Khalfan maana yeye alianza akiwa mduchu haswa, watu wazima wa mtaani walikua wakimuamini na kumpa namba kwenye karibia kila mchezo. Habari hii haikupokelewa vyema na Mzee wake ambaye alipiga STOP nyendo hizo za mwanaye kitu kilocho sababisha wazee wa mtaa wajipange na kuandamana kwenda kwa Baba yake Nizar kumuombea ruhusa midfielder maestro aachiwe na kwenda kutoa burudani. Kama ilivyokua kwa mzazi yoyote, uzito kwenye maisha ya Nizar ulikua ni elimu zaidi na hapo ndipo Baba yake alipotaka mwanaye apakazie sana. Haikuchukua muda Nizar kuonekana na team nyengine na pia kuitwa kwenye team ya Taifa ya vijana ambako kipaji chake kiling’ara kama mwezi ulotimia. Akatoka team moja kwenda nyengine mpaka safari ya Canada ilipoiva! Haikua rahisi pia kama unavyodhani maana masuala ya visa zaidi ndo yalionekana kuchukua muda mpaka kama Nizar alikata tamaa hivi ila Mungu ni mwema, mzigo ukatoka na safari ya Vancouver ikaanza. Maongezi haya zaidi ni kuhusu huko Canada, mpaka akarudi na kuanzia Yanga ingawa chaguo la kwanza lilikua Simba ila watu walizidiana kete na ujanja na mwisho wa siku kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania aliishia Jangwani kwa miaka kadhaa kabla hajahamia Singida. Mimi nilitaka kujua zaidi hiyo safari na kipi haswa kilimfanya achague Yanga (hii ni personal kidogo 😀) na challenges alizowahi kupata akiwa ugenini. Maisha baada kurudi nyumbani, mustakabali wa watu kuitwa ‘wazee’ wakati bado umri wao unaruhusu kukipiga daraja la juu na maisha yake kama yeye. Mwaka huu Nizar alimpoteza mke wake (Mwenyezi Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi) baada ya kuugua si kwa muda mrefu. Nizar atatuelezea kilichotokea, na vile vile kuna challenges kama binadamu wa kawaida alizipitia. Haikua rahisi sana kuongelea kila kitu ila ilikua vyema sana kuongea nae na kujua pia plans zake za mbeleni. Yangu matumaini utaelewa na kujifunza jambo! Love, Salama. Soundtrack Yeah by @MarcoChali /watch/QLnf4BH1euC1f Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Category

Show more

Comments - 35