Duration 11:55

Je Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito husababishwa na Nini | Mambo gani hupunguza Maumivu ya Mbavu

15 315 watched
0
163
Published 12 Dec 2021

Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito husababishwa na Nini, Na suluhisho lake ni lipi? Kwa kawaida Kutokana na Mabadiliko mbalimbali ya Kipindi cha Ujauzito, Mjamzito anaweza kuwa na Dalili za kuwa na Maumivu ya Mwili ikiwemo Maumivu ya Mbavu inawezekana Mbavu za Kushoto,Kulia au Pande zote Mbili za Kifua. Hali ya kuwa na Maumivu ya Mbavu katika kipindi cha Ujauzito huweza kupelekea Mjamzito kushindwa Kulala na kupata Usingizi wa Kutosha hivyo huweza kuathiri Afya ya Mama Mjamzito na pia Mtoto aliyeko Tumboni. Tatizo la Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito huwezi kujitokeza Miezi Mitatu ya Mwanzoni, Katikati au Mwishoni mwa Ujauzito na Baadhi ya Wajawazito hupata Maumivu ya Mbavu Upande wa Kulia wa Kifuani kuliko Upande wa Kushoto. MAMBO YANAYOPELEKEA MAUMIVU YA MBAVU KWA MJAMZITO. Baadhi ya Visababishi vya Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito ni kama vifuatavyo; 1. Mabadiliko ya Homoni ktk Kipindi cha Ujauzito. Kutokana na Ongezeko la Homoni za Progesterone, Estrogen na Relaxin huweza kupelekea kulegezwa kwa Tishu na Nyuzi mbalimbali mfano; Ligamenti ambapo huweza kupelekea Msukumo wa Mbavu kwenda juu au Mbele Kifuani,Msukumo au Mjongeo huo huweza kupelekea Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito. 2. Ukuaji wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito, Kadiri Mtoto anavyoongezeka Tumboni mwa Mjamzito,Mfuko wa Uzazi huongezeka pia ambapo huweza kupelekea Shinikizo Kubwa kwenye Mbavu na kupelekea Mjongeo wa Mbavu na Baadhi ya Tishu nyingine hivyo huweza kupelekea Maumivu katika Kipindi cha Ujauzito. 3. Shinikizo Kubwa ambalo huwekwa kwenye Msuli unaohusika na Upumuaji uitwao Diaflamu na kupelekea Maumivu katika Kipindi cha Ujauzito ambapo Wakati mwingine Maumivu huweza kuuma kwenye Ncha ya Bega la Kulia Dalili hii hufanana na Dalili ya Mimba iliyotungwa Nje ya Mji wa Uzazi na kupasuka kupelekea Damu kumwagika kwenye uwazi uliopo Tumboni uitwao Peritoneal Cavity na Msuli huu wa Diaflamu na kusababisha Maumivu kwenye Ncha ya Bega la Kulia. 4. Shida za Mmeng'enyo na Kiungulia, Kutokana na Mabadiliko ya Homoni katika Kipindi cha Ujauzito hususani Ongezeko la Homoni ya Progesterone katika Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito, hupelekea ulegevu wa Mlango unaounganisha Koo la Chakula na Tumbo la Chakula hivyo hupelekea Chakula chenye Mchanganyiko wa Tindikali kurudi kwenye sehemu ya Chini ya Koo la Chakula ambapo huunguza sehemu hiyo na kupelekea Maumivu kwenye Chembe ya Moyo na Wakati mwingine Maumivu hayo hususisha Mbavu na sehemu ya Mgongoni kwa Mjamzito! 5. Ugonjwa wa UTI, Baadhi ya akina Mama Wajawazito hupata Maumivu ya Mbavu ambayo huambatana na Maumivu ya sehemu za Pembeni mwa Tumbo la Mjamzito, Kupata Maumivu wakati wa kukojoa au Kupata Moto Wakati wa Haja ndogo. Hivyo huhitaji kufanyiwa vipimo vya UTI ili kupata Matibabu stahiki. 6.Ukuaji wa Matiti na Ukauji wa Tumbo hupelekea Uzito kuelekea Chini kutokana na Kani ya Uvutano wa Dunia huweza kupelekea kubadilika kwa Mkao wa Mwili na Uti wa Mgongo na hupelekea Mvutiko wa Mabega na Mwili kwenda chini hivyo hupelekea Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito. 7. Maumivu ya Mbavu wakati mwingine husababishwa na kulalia Upande Mmoja wa Mwili kwa Muda mrefu hivyo unahitaji kubadili Upande mwingine wa Kulalia ili kuondokana na Maumivu katika kipindi chake Cha Ujauzito. KUMBUKA: Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito huwa ni hali ya kawaida kutokana na Mabadiliko mbalimbali ya kipindi cha Ujauzito ambapo huweza kupona yenyewe bila Matibabu au Dawa za Maumivu. MAMBO YA KUFANYA ILI KUPUNGUZA MAUMIVU YA MBAVU KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. Ili kuweza kupunguza Maumivu ya Mbavu katika Kipindi Cha Ujauzito unatakiwa kufanya Mambo yafuatayo; 1. Hakikisha una Kaa kwa Mkao wa Wima, Nyoosha Mgongo rudisha Mabega Nyuma na inua Kichwa juu hupunguza Maumivu ya Bega na Mbavu kwa Mjamzito. 2. Hakikisha unavaa Nguo zinazoacha Mwili kuwa huru kuliko Kubana Mwili,hivyo Mjamzito unatakiwa uvae Dela na Brazia ambazo hulegeza Mwili katika kipindi cha Ujauzito. 3. Unatakiwa kufanya Mazoezi ya kulegeza Mwili wako katika kipindi cha Ujauzito. 4. Badili Upande mwingine ambao hauumi endapo Upande ulio lala unapata Maumivu katika upande ulio lalia. 5. Matumizi ya Dawa za Maumivu Mara baada ya kwenda hospitali katika kipindi cha Ujauzito. 6. Maumivu ya Mbavu kwa Mjamzito wakati mwingine huweza kupona yenyewe mara ya Kujifungua. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp #MaumivuMbavu #DrMwanyika #MamaAfya

Category

Show more

Comments - 195